Showing posts with label AFYA YAKO. Show all posts
Showing posts with label AFYA YAKO. Show all posts

Sunday, 4 March 2018

TYPHOID FEVER/homa ya matumbo

TYPHOID FEVER/homa ya matumbo


Habari za leo ndugu msomaji wa blog ya KUSUDI LAKO. Karibuni katika somo la leo ambapo tunazungumzia ugonjwa wa homa ya tumbo ambao kwa lugha ya kitaalamu unaitwa Typhoid umezoeleka kwa jina la TAIFODI

UTANGULIZI

Typhoid ni nini?
Typhoid au Enteric fever au Homa ya matumbo ni ugonjwa wa tumbo unaoenezwa na Bacteria/vimelea waitwao Salmonella Typhi (Typhi ndipo jina Typhoid limepatikana)

MAAMBUKIZI

Kama nilivyo eleza awali katika utangulizi, Typhoid au homa ya matumbo ni ugonjwa unaosababishwa na Bacteria aitwae Salmonella Typhi.

Bacteria ni vimelea au viumbe wadogo sana wanaoweza kusababisha magonjwa na mfano wa magonjwa yanayoenezwa na Bacteria ni Tonsilitis/matezi,Urinary tract infection/UTI,Pneumonia au homa ya mapafu.Otitis media/maskio kutoa usaha..... nakadhalika.

Salmonella mdudu anaesababisha Typhoid hupatikana hasa mazingira yenye bakteria hawa na mara nyingi watu huupata kupitia maji yasiochemshwa na yenye vimelea wa Salmonella. pia hali ya matumizi mabaya ya vyoo na usafi duni (poor sanitation), hivyo basi jihadhari na ulaji wa Vitu kama kachumbari usizojua utengenezaji wake, pia jitahidi kuosha matunda kwa maji yaliochemshwa, kukausha vyombo vya kulia, kufuta mikono au kukausha baada ya kunawa wakati wa kula, kunywa maji yaliochemshwa au kutibiwa isipokua ya mvua

DALILI

1.Homa/fever hali ya mwili kupata joto
2.Body malaise-mwili kuchoka na kukosa nguvu
3.Abdominal pain-tumbo kuuma au kuunguruma na wakati mwingine kuharisha
Hii pia huweza kusababisha kuhara damu kama haitatibika mapema sababu wadudu hutoboa utumbo(intestinal perforation)
4.Headche-kuumwa kichwa
nakadhalika
5.Joints Pain/kuumwa viungo vya mwili
6.Nausea and vomiting sometimes/kichefuchefu na kutapika wakati mwingine(SIO LAZIMA)

VIPIMO

Typhoid hupimwa kwa kipimo kinaitwa Widal test under titration method ambacho huelezea kiwango cha wadudu katika damu
Mfano STH 1:80, STO 1:320
TIBA

Typhoid hutibika vizuri japo tiba haikupi kinga na unaweza ugua tena kama hutozingatia kanuni za Afya
Mfano wa dawa ambazo hutibu ni

Ciprofloxacin
Norfloxacin
Levofloxacin
Cefalexin
Ceftriaxone
Amoxycilline na kadhalika

USHAURI

Usinunue dawa na kumeza bila kupima ama ushauri wa daktari kwani wataalamu na vipimo ndivyo vinaweza kutofautisha homa na magonjwa tofauti tofauti.

AHSANTENI NA KARIBUNI KWA MASWALI.

DR. James
0763 832798
jamesmakala40@gmail.com

Truth about success

Wednesday, 7 February 2018

CHAKULA CHAKO NI DAWA.

“KIFANYE CHAKULA KIWE DAWA YAKO NA DAWA YAKO IWE CHAKULA”
By Hippokrates 460KK-370KK Larisa - Ugiriki


Huu ni msemo uliosemwa na mtaalamu wa kiwango cha juu kabisa katika kada ya utabibu (udaktari) na alijulikana kama baba wa uganga (father of medicine) na hata leo waganga hufuata kiapo kinachosemakana kilitungwa na Hippokrates. Anafahamika kwa mtindo wake wa kuangalia magonjwa uliokuwa ni mpya wakati ule.

Hakuamini tena kuwa ugonjwa unasababishwa na mapepo au uchawi na kurogwa, alichunguza na kugundua kuwa magonjwa mengi yanasababishwa na matatizo ndani ya mwili. Ndipo baadae alipokuja na msemo wake huo hapo juu kwamba
  

“kifanye chakula kiwe dawa yako na dawa yako iwe chakula”


                    Picha ya Hippokrates (baba wa uganga)

Kimsingi chakula tunachokula kinasababisha matokeo makubwa sana katika afya zetu pamoja na uwezo miili yetu kuendelea kuishi, haijalishi kama unajua hili ama haujui matokeo ya kile unachokula yatatokea tu. Kuwa na ufahamu zaidi juu ya masuala ya mlo na sifa za uponyaji utokanao na vyakula, utakusaidia kufanya mabadiliko katika suala zima la ulaji ili uweze kufikia mahitaji ya mwili wako. Na hii itakusaidia kwa kiwango kikubwa kuimarisha na kuboresha afya yako.


NGUVU YA ULINZI KATIKA CHAKULA.

Sayansi mlo (nutritional science) imeangazia zaidi katika umuhim wa chakula kisichotengenezwa viwandani (whole food) :

kutoka hapo tunaelewa kuwa virutubisho vilivyomo ndani ya chakula vinafanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha afya zetu— ambapo vyakula vya kusindikwa (processed food) vinapoteza kiasi kikubwa cha virutubisho, na vinaweza kusababisha magonjwa.

Tujue kuwa vitamin, amino asidi, madini, na mafuta ya muhimu takribani 50 kwa idadi au zaidi zinahitajika katika kila mlo tunaoupata. Na zaidi ya virutubisho-mimea (phyto-nutrients) 1200 vinapatikana katika matunda, mbogamboga, mbegu na vyakula vitokanavyo na wanyama.


Itaendelea….

Dr. James Makala.
0763 832798

© truth about success