Tuesday, 30 January 2018




Dr. James Makala.
0763832798

Truth about success

Tafakari


"Wakati mwingine ukiona watu waliokuwa karibu nawe hawako karibu nawe tena usihangaike, ujue hauna jambo jipya ni muhimu kufanywa upya kila siku ili uwe wa faida na Mungu atukuzwe kupitia wewe. Nao watakufuata”


Dr. James Makala.
0763 832798


© truth about success 

Monday, 29 January 2018

KWA NINI HATUONI MAMBO MAPYA KATIKA MAISHA YETU?

 Bwana yesu asifiwe ninamshukuru Mungu atupaye kushinda na zaidi ya kushinda kila siku. Kuna vitu vichache ambavyo ningependa kukushirikisha kwa sikuya leo.


 KWANINI HATUONI MAMBO MAPYA KATIKA MAISHA YETU.

Tukisoma neno la Mungu tunagundua kuwa kuna mambo mema ambayo Mungu anatuwazia na anatuahidi katika maisha yetu kila siku.

Kwa mfano tukiangalia hapa maneno haya hapa chini…
Yer. 33:3 “ Niite, nami nitakuitikia, na kukuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua”
Yer. 32: 26-27 “ Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia, kusema, tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?
Kumb. 4:7 “ Kwa maana liko taifa gani , lililo na Mungu aliye karibu nao kama Bwana, Mungu wetu,  alivyo, kila tumwitapo”
1 Sam. 7:23 “ Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako, kama Israel, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwqaajili yake, wawe watu wake mwenyewe,  akajifanyie jina, na kutenda mambo makuu kwaajili yenu, na mambo ya kuogofya kwaajili ya nchi yako, mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri wawe wako, kutoka katika mataifa na miungu yao.”

Haya ni maneno ya Mungu ambayo anayotuambia sisi, ni maneno yanayotutamkia kwenda mbele na kuinuliwa, lakini sasa kwa nini hatuoni mambo mapya wakati ameahidi kutuonyesha mambo makubwa na magumu tusiyo yajua?
Kumbuka kwamba yeye Mungu/Kristo anatuambia kupitia neno lake kuwa  tuombe bila kukoma (1Thes 5:17), kwa nini alituambia kuomba kama alijua hatakuwa na muda wa kujibu hayo tunayomuomba?
Lakini pia siyo tu alitugiza kuomba lakini pia aliahidi kujibu maombi yetu kimetokea nini leo hatuoni hayo aliyo ahidi?  
Roho Mtakatifu aliyenipa kuandaa somo hili japo kwa ufupi ndiye atakaye tupa majibu ya nini kilichotokea/kinachotokea hata hatuoni mambo mapya katika maisha yetu. Angalia ahadi ya Mungu katika Biblia juu ya kuomba na ahadi yake ya  kujibu maombi yetu. Kabla ya kuangalia mungu alivyoagiza tuombe na ahadi yake ya kujibu maombi hebu kwa kifupi tujifunze nini maana ya maombi/ kuomba.
Mt. 6:7-8; 32 “ Basi msifanane na hao; maana baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba” 32 “ Kwa maana hayo yote mataifa huyatafuta; kwa sababu baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote”


MUNGU ALIAGIZA TUOMBE NA ALIAHIDI KUJIBU MAOMBI YETU

Mwa. 18:17 “ Bwana akanena, je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo”
Zab. 25:14 “ Siri ya Bwana iko kwao wamchao, naye atawajulisha agano lake”
Amo.3:7 “ Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi ake mabii siri yake”
Kum. 4:7 “ Kwa maana liko  Taifa gani kubwa lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo”
Zab. 50:15 “ Ukaniite siku ya mateso; nitakuokoa na wewe utanitukuza”
Yer. 29:12 “  Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza”
Mdo. 2:21 “  Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa”


KUNA SABABU ZA KUTOONA MAMBO MAPYA KATIKA UKRISTO

1. KUOMBA VIBAYA

yak. 4:3 “  Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tama zenu.

” Soma vizuri hapo kuna mtumishi aliniomba nimfundishe kupiga kinanda akasema “kaka namwomba Mungu nikijua kina Fulani watanikoma” nikamwambia hapana huwezi kufanikiwa hivyo…lakini akawa anarudia kauli ile ile kwa akijua wata….. basi mpaka leo ni mwezi wanne nimemfundisha hadi chord za wapi kuleee….lakini hajapata kujua hata wimbo wa kuabudu mrahisi hawezi…wiki iliyopita alikubali nikamwambia utubu sasa na ubadilishe kauli kuwa utajifunza kwa utukufu wa Mungu…nimemuona leo anaendelea vizuri sana anasema anafanya kwa utukufu wa Mungu sasa…nimetoa mfano hai ili uone wakati gani walokole tunakosea uwasaidie na wanaokuzunguka. Anaglia hapa chini….

-yak. 4:15 “Badala ya kusema, Bwana akipenda,  tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi”

1Yn. 5: 14-15 “ Na huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa , tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chochote, twajua ya kwamba tunazo zile haja tulizo mwomba”

Mt. 26:39, 41, 44 “ Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; wala si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; Roho I radhi lakini mwili ni dhaifu. 44 akawaacha tena, akaenda, akaomba mara tatu, akisema maneno yaleyale”
Tuanza kuomba vizuri


2. KUTOOMBA KWA BIDII

Suala la kuomba wote tunafahamu sana lakini shida inatokea pale tunapokata tamaa angalia mfano huu

Lk. 11:5-10 “Akawaambia, ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu amefika kwangu, atoka safarini, name sina kitu cha kuweka mbele yake; na Yule wa ndani amjibu akisema usinitaabishe mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe? Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadri ya haja yake.

Yesu alitoa mfano wa mtu asiyekata tamaa kugonga mlango.. tujifunze kuomba hadi jambo litokee au hadi roho mtakatifu  akuambie yatosha…
Angalia pia hapa….

 Lk.18:1 “ Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa” 

Kum. 4:29 “ Lakini huko kama mkimtafuta, Bwana, Mungu wako utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote na roho yako yote”

Nadhani umeona kwa bidi inahitajika kw asana tu

3. KUTOOMBA KWA IMANI

Mimi sina maelezo mengi sana lakini naomba usikie neno linasema
ebr.11:1 “ Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”

Ebr. 11:6 “  Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”

Yak. 1:6-7 “  Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama Yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana”

Mr. 11:24 “ kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu”

Mt. 7: 7-11 “ Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?”

Yoh. 14:13 “ Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya ili baba yangu atukuzwe ndani ya mwana”

Yon. 16:23 “ Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amini, amini, nawaambia,mkimwomba baba neno lolote kwa jina langu atawapa”


4. DHAMBI.

Isa. 59:1-2 “ Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa; wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kusikia”
hapa sitazungumza sana kwa habari ya kuokoka. Kwa ufupi tu maana ya kuokoka ni kuachana na dhambi simamia vizuri kabisa wokovu Paulo anasema ni kupiga vile vita vizuri vya Imani 1tim 1:18

pamoja na kuokoka kuna dhambi ambazo bado watu wameshikilia na wanasema ni vidhambi vidogo vidogo, kama wivu mbaya wa kuona ukimsaidia mwenzio atakuzidi, hasira, masengenyo, chuki, viuongo uongo ..eti uko mtaa wa Tanzania unaulizwa kwenye simu uko wapi? unasema niko Kenya…  acha uongo huo. kumbuka kuwa pale ulipo kuna watu wanakuangalia wewe kama barua ya kusomwa na wao (2Kor 3:2)…. Nuru yetu na iangaze mbele ya watu wayaone matendo yetu mema. Mat 5:16

basi kwa maneno haya mbarikiwe sana nimepewa kusema hivyo kwa uchache. Mungu akubariki unapoendelea kuyatekeleza haya…”ukiona watu waliokuwa karibu nawe wanajitenga nawe ujue hauna jambo jipya ni muhimu kufanywa upya kila siku ili Mungu atukuzwe kupitia wewe.” katika haya naamini kabisa kwamba lipo jambo la kukusaidia kusogea hatua Zaidi mbele…

Mungu akubariki sana
Dr. James Makala.
0763 832798

© truth about success


Monday, 22 January 2018

HAKI NA UPENDO.

Bwana Yesu asifiwe watumishi wa Bwana wa majeshi, tunamshukuru Mungu atupaye kushinda na zaidi ya kushinda. Ni wakati mwing ine tena tushirikishane maneno ya Mungu. Kadri tunavyoendelea kujifunza na kumtukuza Mungu wetu aliye hai, tuangalie kitu hiki kinachofanya tuendelee kuwepo hapa DUNIANI.

Kichwa cha somo kinaitwa HAKI NA UPENDO.

kwa kuanza tusome  ZABURI 133 neno linasema

"1.Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja.
  2. Ni kama mafuta mazuri kichwani, yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni . yashuikayo mpaka upindo wa mavazi yake.
  3.Kama umande wa Hermoni ushukao mlimani pa sayuni. Maana ndiko bwana alipoamuru Baraka, naam hata uzima wa milele."

Hebu tuangalie kidogo maana ya maneno haya mawili; VYEMA  &  KUPENDEZA.

Maana ya neno VYEMA
Neno hili linatokana na neno vema
 maana yake ni jambo/kitu sahihi,kilicho haki, kilicho sawa, inavyopaswa kuwa nk.

Maana neno PENDEZA…
Neno hili lina neno penda ndani yake..wanaokumbuka  Kiswahili  katika vitenzi kuna vitenzi vinaitwa vitenzi nomino yaani ni kitendo ambacho asili yake kimetokana na jina kama kupenda kunatokana na neno upendo,

sasa kutokana na neno PENDA hiki ni kitendo lakini kikiongezwa kiambishi tamati –ez- kitalifanya neno liwe katika hali ya kutendesha… kwa hiyo PENDEZA ni kitenzi kitendeshi.
Kwa maelezo hayo  pendeza ni kitendo cha kusababisha upendo juu ya kitu Fulani. Kwa mfano ukiona mtu amependeza ina maana kwamba kuna jambo alimefanya linalosababaisha umpende au ukipende ndio maana mtu hukazia  “yaani nguo/viatu/gari/ bustani..nk  imependeza kweli nimeipenda”
Popote panapopendeza kuna Upendo…

 Sasa basi wale tuliobahatika kusoma chekechea si  tunakumbuka siku tulikuwa tukipata vema maswali yote, tulikuwa tunafanyiwa kasherehe ka kupewa pipi, ubuyu, dengu vibalagala n.k...ni kwa sababu tulikuwa tumefanya jambo jema ..na jambo hilo lilipendeza na kuwafanya watu watupende lakini sio kutupenda tu hata watupatie zawadi nk. Na ndipo tulikuwa tunafurahia sana ule ushindi tulioupata katika yale tuyafanyayo. Kama baba alivyofanya asubuhi ni kwa sababu kulikuwa na kuna jambo jema  likampendeza mpaka akasukumwa kutoa zawadi..

Kumbe kufanya jambo lililo vyema/ haki  kunaleta kupendeza/upendo.
Kwa hiyo nikimsikia Muheshimiwa Mfalme DAUDI anasema VYEMA NA KUPENDEZA  ninapata maana kuwa anasema  HAKI NA  UPENDO. Sasa kumbuka ukiona neno utakapoona mahali pameandikwa
VYEMA=HAKI  au KUPENDEZA = UPENDO.
Bila shaka utakubaliana nami kwa ufafanuzi wa utangulizi niliotoa.

Tuangalie kwenye vipengele vichache vifuatavyo kabla niende kukesha hukoo kanisani…
a.       Muanzilishi wa haki na upendo.
b.      Umuhimu/ ulazima wa Haki na upendo.
c.       Faida za haki na upendo.
d.      Hasara za kutokutenda haki na upendo.

A.      MUANZILISHI WA HAKI NA UPENDO .
Mungu ndiye muhasisi au muweka jiwe la msingi la haki na upendo maana yeye ndiye HAKI NA UPENDO  fuatilia hapa…

1.HAKI
i. Mungu ndiye mmiliki wa haki
Isaya  45:21…ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, Bwana? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi, Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.

Utaona anaitwa  MUNGU WA HAKI., zaburi  4;1

Kwa maana , wakiwa hawaijui haki ya Mungu na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe , hawakujitia chini ya HAKI YA MUNGU…Rum 10;3


ii. Mungu ndiye awezaye kuwahesabia haki watu.
tukihesabiwa haki na MUNGU tuko salama maana yeye ndiye mmiliki wa haki hakuna awezaye kutushitaki…..…ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki..8:33

2. UPENDO.
i. Mungu mwenyewe ni upendo.
Yeye asiyependa hakumjua Mungu maana Mungu ni Upendo…1 yoh 4:8.

Sikia hapa MUNGU =UPENDO 

Yaani mtu ambaye hajaokoka akikuambia anakupenda, ujue anakudanganya ni kwamba amekutamani  tu, ambao hawajaokoka hawajui kupenda maana MUNGU ambaye ni UPENDO
hayumo ndani yao……nasi tumelifahamu pendo alilonalo Mungu kwetu sisi na kuliamini. Mungu nu upendo, naye akaaye katika pendo hukaa ndani ya Mungu, na Mungu ndani yake. so be Eyes everyone.

B.      UMUHIMU AU ULAZIMA WA HAKI NA UPENDO.

1.       NI AMRI KUU YA MUNGU.
Marko 12:30-31
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote… na ya pili ndio hii, mpende jirani yako kama nafsi yako. “HAKUNA AMRI ILIYO KUU KULIKO HIZI”
YESU alikuwa smartmind sana, maana wayahudi walikuwa wanajifanya wanajua sana amri za Mungu na maandiko lkn walikuwa hawayaishi yale waliyoyameza.… kwa hiyo Yesu aliwaambia kuwa wanapotea kwa sababu hawajui uweza wa Mungu uliomo katika neno la Mungu… sasa kurahisisha akafanya summary ya amri zote 10 zikawa 2 tu.  Kwa kisukuma  wanasema 10 in 2.

2.       UPENDO NA HAKI HUAMBATANA
Kama tulivyoona hapo juu lengo kubwa la amri za Mungu ambazo zimefichwa ndani ya UPENDO dhamira yake ni kuleta HAKI ndio maana somo linaitwa HAKI NA UPENDO . maana PALIPO NA HAKI KUNA UPENDO PALIPO NA UPENDO KUNA  HAKI.
Zaburi 133.

3.       PASIPOKUWA NA UPENDO HAIWEZAKANI KUMPENDEZA MUNGU.
Nijaposema kwa lugha zote za wanadamu na za malaika kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao…
Kichwa cha habari chajieleza. Nasi twajua mungu baba, mungu mwana naye roho mtakatifu wako katika hali ya upendo ndio maana hakuna kitendeacho kazi pasipo kujulikana kwa sehemu zingine..


itaendelea....

Mbarikiwe sana.
Dr. James
               0763 832798
               Jamesmakala40@gmail.com

               © truth about success