Bwana yesu asifiwe ninamshukuru Mungu atupaye
kushinda na zaidi ya kushinda kila siku. Kuna vitu vichache ambavyo ningependa
kukushirikisha kwa sikuya leo.
KWANINI HATUONI MAMBO MAPYA KATIKA MAISHA
YETU.
Tukisoma
neno la Mungu tunagundua kuwa kuna mambo mema ambayo Mungu anatuwazia na
anatuahidi katika maisha yetu kila siku.
Kwa mfano tukiangalia
hapa maneno haya hapa chini…
Yer. 33:3 “ Niite, nami nitakuitikia, na kukuonyesha
mambo makubwa, magumu usiyoyajua”
Yer. 32: 26-27 “ Ndipo neno la Bwana
likamjia Yeremia, kusema, tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je!
Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?
Kumb. 4:7 “ Kwa maana liko taifa gani
, lililo na Mungu aliye karibu nao kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo”
1 Sam. 7:23 “ Tena ni taifa lipi
duniani lililo kama watu wako, kama Israel, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa
kwqaajili yake, wawe watu wake mwenyewe,
akajifanyie jina, na kutenda mambo makuu kwaajili yenu, na mambo ya
kuogofya kwaajili ya nchi yako, mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri
wawe wako, kutoka katika mataifa na miungu yao.”
Haya ni
maneno ya Mungu ambayo anayotuambia sisi, ni maneno yanayotutamkia kwenda mbele
na kuinuliwa, lakini sasa kwa nini hatuoni mambo mapya wakati ameahidi
kutuonyesha mambo makubwa na magumu tusiyo yajua?
Kumbuka kwamba
yeye Mungu/Kristo anatuambia kupitia neno lake kuwa tuombe bila kukoma (1Thes 5:17), kwa nini
alituambia kuomba kama alijua hatakuwa na muda wa kujibu hayo tunayomuomba?
Lakini pia
siyo tu alitugiza kuomba lakini pia aliahidi kujibu maombi yetu kimetokea nini
leo hatuoni hayo aliyo ahidi?
Roho Mtakatifu
aliyenipa kuandaa somo hili japo kwa ufupi ndiye atakaye tupa majibu ya nini
kilichotokea/kinachotokea hata hatuoni mambo mapya katika maisha yetu. Angalia
ahadi ya Mungu katika Biblia juu ya kuomba na ahadi yake ya kujibu maombi yetu. Kabla ya kuangalia mungu
alivyoagiza tuombe na ahadi yake ya kujibu maombi hebu kwa kifupi tujifunze
nini maana ya maombi/ kuomba.
Mt. 6:7-8;
32 “ Basi msifanane na hao; maana baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi
hamjamwomba” 32 “ Kwa maana hayo yote mataifa huyatafuta; kwa sababu baba yenu
wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote”
MUNGU ALIAGIZA TUOMBE NA ALIAHIDI
KUJIBU MAOMBI YETU
Mwa. 18:17 “
Bwana akanena, je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo”
Zab. 25:14 “
Siri ya Bwana iko kwao wamchao, naye atawajulisha agano lake”
Amo.3:7 “
Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi ake mabii
siri yake”
Kum. 4:7 “
Kwa maana liko Taifa gani kubwa lililo
na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo”
Zab. 50:15 “
Ukaniite siku ya mateso; nitakuokoa na wewe utanitukuza”
Yer. 29:12
“ Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba,
nami nitawasikiliza”
Mdo. 2:21
“ Na itakuwa kila atakayeliitia jina la
Bwana ataokolewa”
KUNA SABABU ZA KUTOONA MAMBO MAPYA
KATIKA UKRISTO
1. KUOMBA VIBAYA
yak. 4:3 “ Hata mwaomba, wala
hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tama zenu.
” Soma vizuri hapo kuna mtumishi aliniomba nimfundishe kupiga kinanda
akasema “kaka namwomba Mungu nikijua kina Fulani watanikoma” nikamwambia hapana
huwezi kufanikiwa hivyo…lakini akawa anarudia kauli ile ile kwa akijua wata…..
basi mpaka leo ni mwezi wanne nimemfundisha hadi chord za wapi kuleee….lakini
hajapata kujua hata wimbo wa kuabudu mrahisi hawezi…wiki iliyopita alikubali
nikamwambia utubu sasa na ubadilishe kauli kuwa utajifunza kwa utukufu wa
Mungu…nimemuona leo anaendelea vizuri sana anasema anafanya kwa utukufu wa
Mungu sasa…nimetoa mfano hai ili uone wakati gani walokole tunakosea uwasaidie
na wanaokuzunguka. Anaglia hapa chini….
-yak. 4:15 “Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi”
1Yn. 5: 14-15 “ Na huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa , tukiomba
kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia,
tuombacho chochote, twajua ya kwamba tunazo zile haja tulizo mwomba”
Mt. 26:39, 41, 44 “ Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli,
akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; wala si kama
nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia
majaribuni; Roho I radhi lakini mwili ni dhaifu. 44 akawaacha tena, akaenda,
akaomba mara tatu, akisema maneno yaleyale”
Tuanza kuomba vizuri
2. KUTOOMBA KWA BIDII
Suala la kuomba wote tunafahamu sana lakini shida inatokea pale
tunapokata tamaa angalia mfano huu
Lk. 11:5-10 “Akawaambia, ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku
wa manane, na kumwambia, rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, kwa sababu
rafiki yangu amefika kwangu amefika kwangu, atoka safarini, name sina kitu cha
kuweka mbele yake; na Yule wa ndani amjibu akisema usinitaabishe mlango
umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka
nikupe? Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake,
lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadri ya haja yake.
Yesu alitoa mfano wa mtu asiyekata tamaa kugonga mlango.. tujifunze
kuomba hadi jambo litokee au hadi roho mtakatifu akuambie yatosha…
Angalia pia hapa….
Lk.18:1 “ Akawaambia mfano, ya
kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa”
Kum. 4:29 “ Lakini huko kama mkimtafuta, Bwana, Mungu wako utampata,
ukimtafuta kwa moyo wako wote na roho yako yote”
Nadhani umeona kwa bidi inahitajika kw asana tu
3. KUTOOMBA KWA IMANI
Mimi sina maelezo mengi
sana lakini naomba usikie neno linasema
ebr.11:1 “ Basi imani ni
kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”
Ebr. 11:6 “ Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;
kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa
thawabu wale wamtafutao”
Yak. 1:6-7 “ Ila na aombe kwa
imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari,
lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama Yule
asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana”
Mr. 11:24 “ kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote myaombayo mkisali, aminini
ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu”
Mt. 7: 7-11 “ Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni,
nanyi mtafunguliwa;kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye
abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate,
atampa jiwe? Au akiomba samaki atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu,
mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana baba yenu aliye
mbinguni atawapa mema wao wamwombao?”
Yoh. 14:13 “ Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya ili
baba yangu atukuzwe ndani ya mwana”
Yon. 16:23 “ Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amini, amini,
nawaambia,mkimwomba baba neno lolote kwa jina langu atawapa”
4. DHAMBI.
Isa. 59:1-2 “ Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa;
wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu
yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone
hata hataki kusikia”
hapa sitazungumza sana kwa habari ya kuokoka. Kwa ufupi tu maana ya
kuokoka ni kuachana na dhambi simamia vizuri kabisa wokovu Paulo anasema ni
kupiga vile vita vizuri vya Imani 1tim 1:18
pamoja na kuokoka kuna dhambi ambazo bado watu wameshikilia na wanasema
ni vidhambi vidogo vidogo, kama wivu mbaya wa kuona ukimsaidia mwenzio
atakuzidi, hasira, masengenyo, chuki, viuongo uongo ..eti uko mtaa wa Tanzania
unaulizwa kwenye simu uko wapi? unasema niko Kenya… acha uongo huo. kumbuka kuwa pale
ulipo kuna watu wanakuangalia wewe kama barua ya kusomwa na wao (2Kor 3:2)…. Nuru yetu na
iangaze mbele ya watu wayaone matendo yetu mema. Mat 5:16
basi kwa maneno haya mbarikiwe sana nimepewa kusema hivyo kwa uchache.
Mungu akubariki unapoendelea kuyatekeleza haya…”ukiona watu waliokuwa karibu nawe wanajitenga nawe ujue hauna jambo
jipya ni muhimu kufanywa upya kila siku ili Mungu atukuzwe kupitia wewe.”
katika haya naamini kabisa kwamba lipo jambo la kukusaidia kusogea hatua Zaidi
mbele…
Mungu akubariki sana
Dr. James Makala.
0763 832798
© truth about success
No comments:
Post a Comment