Monday, 22 January 2018

HAKI NA UPENDO.

Bwana Yesu asifiwe watumishi wa Bwana wa majeshi, tunamshukuru Mungu atupaye kushinda na zaidi ya kushinda. Ni wakati mwing ine tena tushirikishane maneno ya Mungu. Kadri tunavyoendelea kujifunza na kumtukuza Mungu wetu aliye hai, tuangalie kitu hiki kinachofanya tuendelee kuwepo hapa DUNIANI.

Kichwa cha somo kinaitwa HAKI NA UPENDO.

kwa kuanza tusome  ZABURI 133 neno linasema

"1.Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja.
  2. Ni kama mafuta mazuri kichwani, yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni . yashuikayo mpaka upindo wa mavazi yake.
  3.Kama umande wa Hermoni ushukao mlimani pa sayuni. Maana ndiko bwana alipoamuru Baraka, naam hata uzima wa milele."

Hebu tuangalie kidogo maana ya maneno haya mawili; VYEMA  &  KUPENDEZA.

Maana ya neno VYEMA
Neno hili linatokana na neno vema
 maana yake ni jambo/kitu sahihi,kilicho haki, kilicho sawa, inavyopaswa kuwa nk.

Maana neno PENDEZA…
Neno hili lina neno penda ndani yake..wanaokumbuka  Kiswahili  katika vitenzi kuna vitenzi vinaitwa vitenzi nomino yaani ni kitendo ambacho asili yake kimetokana na jina kama kupenda kunatokana na neno upendo,

sasa kutokana na neno PENDA hiki ni kitendo lakini kikiongezwa kiambishi tamati –ez- kitalifanya neno liwe katika hali ya kutendesha… kwa hiyo PENDEZA ni kitenzi kitendeshi.
Kwa maelezo hayo  pendeza ni kitendo cha kusababisha upendo juu ya kitu Fulani. Kwa mfano ukiona mtu amependeza ina maana kwamba kuna jambo alimefanya linalosababaisha umpende au ukipende ndio maana mtu hukazia  “yaani nguo/viatu/gari/ bustani..nk  imependeza kweli nimeipenda”
Popote panapopendeza kuna Upendo…

 Sasa basi wale tuliobahatika kusoma chekechea si  tunakumbuka siku tulikuwa tukipata vema maswali yote, tulikuwa tunafanyiwa kasherehe ka kupewa pipi, ubuyu, dengu vibalagala n.k...ni kwa sababu tulikuwa tumefanya jambo jema ..na jambo hilo lilipendeza na kuwafanya watu watupende lakini sio kutupenda tu hata watupatie zawadi nk. Na ndipo tulikuwa tunafurahia sana ule ushindi tulioupata katika yale tuyafanyayo. Kama baba alivyofanya asubuhi ni kwa sababu kulikuwa na kuna jambo jema  likampendeza mpaka akasukumwa kutoa zawadi..

Kumbe kufanya jambo lililo vyema/ haki  kunaleta kupendeza/upendo.
Kwa hiyo nikimsikia Muheshimiwa Mfalme DAUDI anasema VYEMA NA KUPENDEZA  ninapata maana kuwa anasema  HAKI NA  UPENDO. Sasa kumbuka ukiona neno utakapoona mahali pameandikwa
VYEMA=HAKI  au KUPENDEZA = UPENDO.
Bila shaka utakubaliana nami kwa ufafanuzi wa utangulizi niliotoa.

Tuangalie kwenye vipengele vichache vifuatavyo kabla niende kukesha hukoo kanisani…
a.       Muanzilishi wa haki na upendo.
b.      Umuhimu/ ulazima wa Haki na upendo.
c.       Faida za haki na upendo.
d.      Hasara za kutokutenda haki na upendo.

A.      MUANZILISHI WA HAKI NA UPENDO .
Mungu ndiye muhasisi au muweka jiwe la msingi la haki na upendo maana yeye ndiye HAKI NA UPENDO  fuatilia hapa…

1.HAKI
i. Mungu ndiye mmiliki wa haki
Isaya  45:21…ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, Bwana? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi, Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.

Utaona anaitwa  MUNGU WA HAKI., zaburi  4;1

Kwa maana , wakiwa hawaijui haki ya Mungu na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe , hawakujitia chini ya HAKI YA MUNGU…Rum 10;3


ii. Mungu ndiye awezaye kuwahesabia haki watu.
tukihesabiwa haki na MUNGU tuko salama maana yeye ndiye mmiliki wa haki hakuna awezaye kutushitaki…..…ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki..8:33

2. UPENDO.
i. Mungu mwenyewe ni upendo.
Yeye asiyependa hakumjua Mungu maana Mungu ni Upendo…1 yoh 4:8.

Sikia hapa MUNGU =UPENDO 

Yaani mtu ambaye hajaokoka akikuambia anakupenda, ujue anakudanganya ni kwamba amekutamani  tu, ambao hawajaokoka hawajui kupenda maana MUNGU ambaye ni UPENDO
hayumo ndani yao……nasi tumelifahamu pendo alilonalo Mungu kwetu sisi na kuliamini. Mungu nu upendo, naye akaaye katika pendo hukaa ndani ya Mungu, na Mungu ndani yake. so be Eyes everyone.

B.      UMUHIMU AU ULAZIMA WA HAKI NA UPENDO.

1.       NI AMRI KUU YA MUNGU.
Marko 12:30-31
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote… na ya pili ndio hii, mpende jirani yako kama nafsi yako. “HAKUNA AMRI ILIYO KUU KULIKO HIZI”
YESU alikuwa smartmind sana, maana wayahudi walikuwa wanajifanya wanajua sana amri za Mungu na maandiko lkn walikuwa hawayaishi yale waliyoyameza.… kwa hiyo Yesu aliwaambia kuwa wanapotea kwa sababu hawajui uweza wa Mungu uliomo katika neno la Mungu… sasa kurahisisha akafanya summary ya amri zote 10 zikawa 2 tu.  Kwa kisukuma  wanasema 10 in 2.

2.       UPENDO NA HAKI HUAMBATANA
Kama tulivyoona hapo juu lengo kubwa la amri za Mungu ambazo zimefichwa ndani ya UPENDO dhamira yake ni kuleta HAKI ndio maana somo linaitwa HAKI NA UPENDO . maana PALIPO NA HAKI KUNA UPENDO PALIPO NA UPENDO KUNA  HAKI.
Zaburi 133.

3.       PASIPOKUWA NA UPENDO HAIWEZAKANI KUMPENDEZA MUNGU.
Nijaposema kwa lugha zote za wanadamu na za malaika kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao…
Kichwa cha habari chajieleza. Nasi twajua mungu baba, mungu mwana naye roho mtakatifu wako katika hali ya upendo ndio maana hakuna kitendeacho kazi pasipo kujulikana kwa sehemu zingine..


itaendelea....

Mbarikiwe sana.
Dr. James
               0763 832798
               Jamesmakala40@gmail.com

               © truth about success



No comments:

Post a Comment