Tuesday, 20 February 2018
Friday, 16 February 2018
TAMBUA KUSUDI LA WEWE KUWEPO HAPA DUNIANI
TAMBUA KUSUDI LA WEWE
KUWEPO HAPA DUNIANI
"Janga kubwa katika
maisha sio kifo bali ni maisha bila kusudi"
Dr. Myles Munroe
Msingi unatoka katika
kitabu cha Yohana 15 : 16
Si ninyi mlionichagua
mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda;
na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu
awapeni.
Twende taratibu sasa....
JAMBO LA KWANZA
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi
niliyewachagua ninyi;
Haya ni maneno ya Yesu ukianza kusoma mistari ya nyuma
utaona alikuwa katika kufundisha...
Yesu ndiye Mungu ambaye ndiye roho mtakatifu Utatu ndani ya
Mungu mmoja...
Huyu ndiye aliyetuweka hapa duniani ndiye aliyesema katika
Mwanzo 1
27 - Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu
alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
NOTE
Tambua kuwa yupo haujajiweka hapa duniani.. aliyekuweka na
ndiye mwenye sababu ya wewe kuishi hapa duniani
JAMBO LA PILI
.nami nikawaweka
mwende mkazae matunda;
Baada ya kuwa
tumechaguliwa au kuumbwa kwa mfano wa Mungu na kujua kwa nini tumeumbwa
tunapaawa kuzaa..
hapa haimaanishi kujifungua...😂😂
Anamaanisha vile
tulivyonavyo tuviongeze/ tuvikuze/ tuvilee au tuviboreshe na tuwafundishe
wengine kuvifanya nao wafanye ili kujenga Ufalme wa Mungu
Tazama Mwanzo 1 : 28
"Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke,
mkaijaze nchi,"
tunapaswa kuanza
kutafuta ni jambo gani unaloweza kulifanya kwa urahisi linalompa Mungu utukufu
na litakalowaleta watu kwa Yesu, hususan kwa karama uliyo nayo. Hapo tutakuwa tunazaa matunda.
NOTE
Tambua karama/vipawa na uwezo ulionao unapaswa utumike
kushare na wengine na kuwaleta wengine kwa Yesu...huko ndiko kuzaa matunda
JAMBO LA TATU
matunda yenu yapate kukaa;
Hapa linazungumziwa suala la uendelevu yale matunda
tunayoyazaa tusiyapoteze tuhakikishe yanaendelea kuwepo siku zote tena nayo
yazae matunda mengine mengi...
Hatupaswi kuchoka katika kuyatunza yale matunda yetu mema
ili yaendelee kukaa nayo yazae..
Wagalatia 6 : 9
"Tena tusichoke katika
kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho."
NOTE
Tambua unapozaa matunda yako hakikisha huchoki kuyatunza
yaani kuyafanya yakae kwenye haki ile ile ya ufresh
JAMBO LA NNE
ili kwamba lo lote
mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Hapa
kuna suprise hapa mmeiona?
kumbe yoote hayo tuliyokuwa
tunayafanya hapo juu yana jambo jema hapa mwisho
Kumbe tukifanya...
1. Kuzaa matunda.
2. Kuyafanya yadumu.
3.Halafu tukimuomuomba Mungu kwa Jina La Yesu tunapewa
Hakuna shida wala matatizo tena ikiwa tutafuata kanuni hii aliyoiweka muumbaji wetu. ndio maana neno anasema katika..
Mathayo 6:33
"Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine
mtazidishiwa."
NOTE
1. Kumzalia Mungu matunda na Kuyafanya yakae ndio kusudi la
Mungu kutuumba.
2. Ndipo penye majibu ya mahitaji yetu yotee
Basi kwa neno hili tuhitimishe hivi...
Kwa wale tunaohangaika na kutumia nguvu sana kuomba hatupati majibu
inawezekana hatujafuata utaratibu/kanuni...
jaribu kuishi kwa utaratibu
huu utapata majibu haraka.
1. Zaa matunda
2. Yafanye yakae
Baada ya hayo omba lolote
sasa.
Mbarikiwe sana.
Dr James Makala
0763 832798
©truth about success
Wednesday, 7 February 2018
CHAKULA CHAKO NI DAWA.
“KIFANYE
CHAKULA KIWE DAWA YAKO NA DAWA YAKO IWE CHAKULA”
By Hippokrates
460KK-370KK Larisa - Ugiriki
Huu ni msemo uliosemwa na
mtaalamu wa kiwango cha juu kabisa katika kada ya utabibu (udaktari) na
alijulikana kama baba wa uganga (father of medicine) na hata leo waganga
hufuata kiapo kinachosemakana kilitungwa na Hippokrates. Anafahamika kwa mtindo
wake wa kuangalia magonjwa uliokuwa ni mpya wakati ule.
Hakuamini tena kuwa ugonjwa
unasababishwa na mapepo au uchawi na kurogwa, alichunguza na kugundua kuwa
magonjwa mengi yanasababishwa na matatizo ndani ya mwili. Ndipo baadae
alipokuja na msemo wake huo hapo juu kwamba
“kifanye
chakula kiwe dawa yako na dawa yako iwe chakula”
Picha
ya Hippokrates (baba wa uganga)
Kimsingi chakula tunachokula kinasababisha
matokeo makubwa sana katika afya zetu pamoja na uwezo miili yetu kuendelea
kuishi, haijalishi kama unajua hili ama haujui matokeo ya kile unachokula
yatatokea tu. Kuwa na ufahamu zaidi juu ya masuala ya mlo na sifa za uponyaji
utokanao na vyakula, utakusaidia kufanya mabadiliko katika suala zima la ulaji
ili uweze kufikia mahitaji ya mwili wako. Na hii itakusaidia kwa kiwango
kikubwa kuimarisha na kuboresha afya yako.
NGUVU YA ULINZI KATIKA
CHAKULA.
Sayansi mlo (nutritional science) imeangazia zaidi katika umuhim wa chakula kisichotengenezwa viwandani (whole food) :
kutoka hapo tunaelewa kuwa
virutubisho vilivyomo ndani ya chakula vinafanya kazi kwa ushirikiano ili
kuboresha afya zetu— ambapo vyakula vya kusindikwa (processed food) vinapoteza
kiasi kikubwa cha virutubisho, na vinaweza kusababisha magonjwa.
Tujue kuwa vitamin, amino
asidi, madini, na mafuta ya muhimu takribani 50 kwa idadi au zaidi zinahitajika
katika kila mlo tunaoupata. Na zaidi ya virutubisho-mimea
(phyto-nutrients) 1200 vinapatikana katika matunda, mbogamboga, mbegu na
vyakula vitokanavyo na wanyama.
Itaendelea….
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Bwana yesu asifiwe ninamshukuru Mungu atupaye kushinda na zaidi ya kushinda kila siku. Kuna vitu vichache ambavyo ningependa kukushirikish...
-
TAMBUA KUSUDI LA WEWE KUWEPO HAPA DUNIANI "Janga kubwa katika maisha sio kifo bali ni maisha bila kusudi" Dr. M...
-
TYPHOID FEVER/homa ya matumbo Habari za leo ndugu msomaji wa blog ya KUSUDI LAKO. Karibuni katika somo la leo ambapo tunazungumzia ugonjw...