Wednesday, 7 February 2018

CHAKULA CHAKO NI DAWA.

“KIFANYE CHAKULA KIWE DAWA YAKO NA DAWA YAKO IWE CHAKULA”
By Hippokrates 460KK-370KK Larisa - Ugiriki


Huu ni msemo uliosemwa na mtaalamu wa kiwango cha juu kabisa katika kada ya utabibu (udaktari) na alijulikana kama baba wa uganga (father of medicine) na hata leo waganga hufuata kiapo kinachosemakana kilitungwa na Hippokrates. Anafahamika kwa mtindo wake wa kuangalia magonjwa uliokuwa ni mpya wakati ule.

Hakuamini tena kuwa ugonjwa unasababishwa na mapepo au uchawi na kurogwa, alichunguza na kugundua kuwa magonjwa mengi yanasababishwa na matatizo ndani ya mwili. Ndipo baadae alipokuja na msemo wake huo hapo juu kwamba
  

“kifanye chakula kiwe dawa yako na dawa yako iwe chakula”


                    Picha ya Hippokrates (baba wa uganga)

Kimsingi chakula tunachokula kinasababisha matokeo makubwa sana katika afya zetu pamoja na uwezo miili yetu kuendelea kuishi, haijalishi kama unajua hili ama haujui matokeo ya kile unachokula yatatokea tu. Kuwa na ufahamu zaidi juu ya masuala ya mlo na sifa za uponyaji utokanao na vyakula, utakusaidia kufanya mabadiliko katika suala zima la ulaji ili uweze kufikia mahitaji ya mwili wako. Na hii itakusaidia kwa kiwango kikubwa kuimarisha na kuboresha afya yako.


NGUVU YA ULINZI KATIKA CHAKULA.

Sayansi mlo (nutritional science) imeangazia zaidi katika umuhim wa chakula kisichotengenezwa viwandani (whole food) :

kutoka hapo tunaelewa kuwa virutubisho vilivyomo ndani ya chakula vinafanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha afya zetu— ambapo vyakula vya kusindikwa (processed food) vinapoteza kiasi kikubwa cha virutubisho, na vinaweza kusababisha magonjwa.

Tujue kuwa vitamin, amino asidi, madini, na mafuta ya muhimu takribani 50 kwa idadi au zaidi zinahitajika katika kila mlo tunaoupata. Na zaidi ya virutubisho-mimea (phyto-nutrients) 1200 vinapatikana katika matunda, mbogamboga, mbegu na vyakula vitokanavyo na wanyama.


Itaendelea….

Dr. James Makala.
0763 832798

© truth about success

No comments:

Post a Comment